31 Desemba 2024 - 04:33
MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA - SOMO LA 2: KIPIMO CHA MAJADILIANO

Kuboresha hali ya maisha na uhusiano inawezekana kwa kutumia kipimo, sehemu mbili ya tatu ni kuwa makini na theluthi moja ni upuuziaji.

Al-Imam Ja'afer as-Sadiq (a.s) amesema : "Kuboresha hali ya maisha na uhusiano inawezekana kwa kutumia kipimo, sehemu mbili ya tatu ni kuwa makini na theluthi moja ni upuuziaji."  Tuhfatul ' Uqul, uk. 267

Maelezo mafupi: 

Hakuna kazi inayoanzishwa bila ya kufanyiwa utafiti, mpango au umakini, na vile vile hakuna kazi ambayo haimaliziki bila ya upuuzaji.

Itakuwa wazi kusema vyema kuwa iwapo sisi tutataka kufanya kazi pasi na uchunguzi au utafiti na umakini, basi sisi kamwe hatutafanikiwa. 

Lakini iwapo sisi tutataka kung'ang'ania kila jambo linaloweza kutokea bila ya kutabiriwa wakati tufanyapo kazi, basi kamwe hatutaweza kufanya kazi zetu kwa uwepesi, na itatubidi tuishie miaka mingi katika kusomea tu kwa ajili ya kufanya jambo au kumchagua rafiki, mke na mambo kama hayo. 

Ndiyo maana inasemwa kuwa sehemu mbili ni za umakini na theluthi moja ni ya kutokuwa makini.

  Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho "MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA" - Ayatullah Makarim Shirazi